Add parallel Print Page Options

12 Yanasema hivi kwa sababu hakuna tofauti kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi. Bwana yule yule ndiye Bwana wa watu wote. Naye humbariki sana kila amwombaye akitaka msaada. 13 Ndiyo, “kila mtu anayemwita Bwana[a] ili kupata msaada, ataokolewa.”[b]

14 Lakini watu watawezaje kumwita Bwana na kupata msaada wake ikiwa hawamwamini yeye? Na watawezaje kumwamini Bwana ikiwa hawajawahi kuzisikia habari zake? Na watawezaje kuzisikia habari zake ikiwa hayupo mtu wa kuwaambia?

Read full chapter

Footnotes

  1. 10:13 anayemwita Bwana Kihalisia, “anayeliita jina la Bwana”, ikimaanisha kuonesha imani katika yeye kwa kumwabudu au kumwomba yeye msaada.
  2. 10:13 Yoe 2:32. Tazama pia Kut 2:23-25.